Shaykh Fawzaan: Yupi Anafaa Kuwa Imaam, Haafidhw Mpunguza Ndevu Au Asiye Haafidhw Lakini Hapunguzi Ndevu?
Yupi Anafaa Kuwa Imaam, Haafidhw Mpunguza Ndevu
Au Asiye Haafidhw Lakini Hapunguzi Ndevu?
Shaykh Swaalih bin Fawzaan Al-Fawzaan (Hafidhwahu Allaah)
SWALI:
Kuna Msikiti ambapo hakuna Imaam rasmi, lakini kuna ndugu wawili wazuri. Mmoja wao amehifadhi Msahafu mzima lakini anafupisha ndevu zake na anaswali huku amevaa suruwali, na mwengine amehifadhi sehemu kubwa ya Qur-aan na ameacha ndevu zake na anavaa mavazi ya kawaida. Yupi katika hawa wawili atangulizwe kuwa Imamu?
JIBU:
Atangulizwe yule ambaye kaacha ndevu zake na anavaa mavazi ambayo ni maarufu wanayovaa watu wa mji. Huyu ndiye atangulizwe kwa kuwa ni bora kuliko huyo wa kwanza.
[Mawqi' Ar-Rasmiy li-Ma'aaliy Shaykh Swaalih bin Fawzaan]