Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Hakuna Dalili Ya Khatwiyb Kusoma Aayah Zinazohusiana Na Maudhui Ya Khutbah
Hakuna Dalili Ya Khatwiyb Wa Ijumaa Kusoma
Aayah Zinazohusiana Na Maudhui Ya Khutbah
Imaam Muhammad bin Swaalih Al-'Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:
"...Lakini hapa kuna mas-alah (ambayo) baadhi ya Maimaam wanayafanya, (nayo ni) pindi (Khatwiyb) anapokhutubu, husoma ndani ya Swalaah zile Aayaat zenye mnasaba nayo (khutbah); hili husemwa kuwa ni bid'ah.
Kwa hakika si vinginevyo, Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akijilazimu kwa kusoma Sabbihisma na Al-Ghaashiyah. Au akisoma (Suwrat) Al-Jumu'ah na Al-Munaafiquwn. Na wala hakuwa akichunga (kusoma Aayah) zenye kuhusiana na maudhui ya khutbah.
[Liqaat Al-Baab Al-Maftuwh, mj. 18, uk. 155]