Imaam Ibn Al-Jawziy: Mjinga Anatambulika Kwa Mambo Sita
Mjinga Anatambulika Kwa Mambo Sita
Imaam Ibn Al-Jawziy (Rahimahu-Allaah)
Imaam Ibn Al-Jazwiy (Rahimahu-Allaah) amesema:
“Mjinga hutambulika kwa mambo sita:
- Hughadhibika ovyo bila sababu.
- Hutoa kwa ambaye hastahiki kupewa.
- Huongea ambayo hayana faida.
- Huamini kila mtu.
- Hutangaza siri wala hatofautishi baina ya rafiki yake au adui yake.
- Kuongea lolote lile linamjia moyoni akidhania kuwa yeye ndiye mwerevu kuliko wote.
[Akhbaar Al-Hamqaa- Wal Mughaffaliyn]
