190-Aayah Na Mafunzo: Unapoamka Tahajjud Sunnah Kusoma Aayah Za Mwisho Suwratul-‘Imraan

Aayah Na Mafunzo

Aal-‘Imraan

Unapoamka Tahajjud Sunnah Kusoma Aayah Za Mwisho Suwratul-‘Imraan

Alhidaaya.com

 

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

إِنَّ فِي خَلْقِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَاخْتِلَافِ اللَّيْلِ وَالنَّهَارِ لَآيَاتٍ لِّأُولِي الْأَلْبَابِ ﴿١٩٠﴾ 

Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi, na mabadiliko ya mfuatano wa usiku na mchana; bila shaka ni Aayaat (ishara, zingatio n.k.) kwa wenye akili. [Aal-'Imraan:]

 

Mafunzo:

 

 

Ni Sunnah kuzisoma Aayah kuanzia hiyo mpaka mwisho wa Suwrah anapoamka mtu usiku kuswali (tahajjud). Pia Mama wa Waumini ‘Aaishah  (رضي الله عنها) aliulizwa kuhusu jambo la ajabu alilolishuhudia kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ‘Aaishah akalia kwanza kisha akasema: Mambo yake yote yalikuwa ya ajabu! Usiku mmoja alikuja karibu na mimi mpaka ngozi yake ikagusa ngozi yangu na akasema: “Huniachi nimuabudu Rabb wangu?” Nikasema: Ee Rasuli wa Allaah! Wa-Allaahi hakika mimi napenda ukaribu wako kwangu na pia napenda mahaba yako, na kwamba napenda usiwe mbali na mimi, na napenda yale yanayokufurahisha. Akasema ('Aaishah): Akainuka na kutumia kiroba cha maji na akafanya wudhuu wala hakutumia maji mengi., kisha akasimama akaswali 'Tahajjud' akalia mpaka ndevu zake zikawa zimerowa. Kisha akasujudu na kulia mpaka akaifanya ardhi irowe. Kisha akalala kwa upande wa kulia mpaka akaja Bilaal kumjulisha Adhaan ya Alfajiri, akamuuliza: Ee Rasuli wa Allaah! Jambo gani linakuliza na hali Allaah (سبحانه وتعالى) Amekwishakufutia madhambi yako yaliyotangulia na yanayokuja? Nabiy(صلى الله عليه وآله وسلم)  akasema: “Ee Bilaal! Nini kinizuie mimi kulia wakati usiku huu Allaah (سبحانه وتعالى) Ameniteremshia Aayah hizi?

 

إِنَّ فِي خَلْقِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَاخْتِلَافِ اللَّيْلِ وَالنَّهَارِ لَآيَاتٍ لِّأُولِي الْأَلْبَابِ ﴿١٩٠﴾ 

Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi, na mabadiliko ya mfuatano wa usiku na mchana; bila shaka ni Aayaat (ishara, zingatio) kwa wenye akili. (mpaka mwisho wa Suwrah hii ya Aal-'Imraan (190-200). Kisha akasema: “Ole wake, yule anayezisoma lakini hatafakari kwayo.” [Al-Bukhaariy, Muslim na wengineo]

 

 

 

 

Share