200-Aayah Na Mafunzo: Fadhila Za Ribaatw Fiy SabiliLLaah
Aayah Na Mafunzo
Aal-‘Imraan
Fadhila Za Ribaatw Fiy SabiliLLaah
Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اصْبِرُوا وَصَابِرُوا وَرَابِطُوا وَاتَّقُوا اللَّـهَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ ﴿٢٠٠﴾
200. Enyi walioamini! Subirini na zidini kuvuta subira na bakieni imara na mcheni Allaah ili mpate kufaulu.
Mafunzo:
Baadhi Ya Maana Ya Ribaatw Na Fadhila Zake:
Kwanza: Kubakia, kuthibitika kuchunga, kulinda mipaka katika Jihaad fiy SabiliLLaah
Pili: Kubakia katika ‘Ibaadah baina ya Swalaah Na Swalaah ya pili.
Fadhila za Ribaatw:
Amesimulia Sahl bin Sa’ad (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ): Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمَ) amesema: “Ar-Ribaatw (kusimama imara katika kulinda mipaka kwenye vita vya Jihaad) ya siku moja kwa ajili ya Allaah, ni bora kuliko dunia na vilivyomo. Na sehemu ndogo katika Jannah (Peponi), kiasi cha ukubwa wa fimbo ya mmoja wenu, ni bora kuliko dunia na yaliyomo ndani yake. Na safari ya asubuhi au ya jioni anayosafiri mja katika Njia ya Allaah, ni bora kuliko dunia na vilivyomo.” [Al-Bukhaariy, Muslim]
Pia: Amesimulia Salmaan (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ): Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمَ) amesema: “Ribaatw (kusimama imara katika kulinda mipaka kwenye vita vya Jihaad) ya siku moja na usiku wake, ni bora (katika malipo) kuliko Swiyaam ya mwezi mzima na Qiyaam (kisimamo cha kuswali usiku) chake. Na mtu akifariki (akiwa katika ribaatw), amali zake zitaendelea kuandikwa, na riziki yake ataendelea kuipata, na atasalimika na fitnah (za kaburi).” [Muslim]