041-Aayah Na Mafunzo: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Alipolia Kusikia Qiraa Cha Aayah Hii
Aayah Na Mafunzo
An-Nisaa
Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Alipolia Kusikia Qiraa Cha Aayah Hii
فَكَيْفَ إِذَا جِئْنَا مِن كُلِّ أُمَّةٍ بِشَهِيدٍ وَجِئْنَا بِكَ عَلَىٰ هَـٰؤُلَاءِ شَهِيدًا ﴿٤١﴾
Basi itakuwaje Tutakapoleta kutoka kila Ummah shahidi, na Tukakuleta (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuwa shahidi juu ya hawa? [An-Nisaa: 41]
Mafunzo:
عن عبد الله بن مسعود رضي الله عنه قال: قال لي النبي صلى الله عليه وسلم ((اقرأ علي)) قلت: يا رسول الله، أقرأ عليك وعليك أُنزلَ؟ قال: ((نعم، إني أحب أن أسمعه من غيري)) فقرأت سورة النساء، حتى أتيت إلى هذه الآية: (( فَكَيْفَ إِذَا جِئْنَا مِنْ كُلِّ أُمَّةٍ بِشَهِيدٍ وَجِئْنَا بِكَ عَلَى هَؤُلاءِ شَهِيدًا )) قال: ((حسبك الآن)) فإذا عيناه تَذْرِفَان.
Amesimulia ‘Abdullaah bin Mas‘uwd (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ): Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمَ) aliniambia: “Nisomee!”. Nikamwambia: Ee Rasuli wa Allaah! Nikusomee na hali (Qur-aan) imeteremshwa kwako? Akasema: “Naam! Lakini mimi napenda kusikia wengine wakiisoma.” Nikasoma Suwratun-Nisaa mpaka nilipofikia Aayah:
فَكَيْفَ إِذَا جِئْنَا مِن كُلِّ أُمَّةٍ بِشَهِيدٍ وَجِئْنَا بِكَ عَلَىٰ هَـٰؤُلَاءِ شَهِيدًا ﴿٤١﴾
“Basi itakuwaje Tutakapoleta kutoka kila ummah shahidi, na Tukakuleta (ee Muhammad صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمَ) kuwa shahidi juu ya hawa?”
Akasema: “Hasbuka! (Inatosha, simama hapo).” Nikaona machozi yamejaa machoni mwake. [Al-Bukhaariy]