038-Aayah Na Mafunzo: Kufedheheshwa Siku Ya Qiyaamah Kwa Mwenye Kufanya ‘Amali Kwa Riyaa
Aayah Na Mafunzo
An-Nisaa
Kufedheheshwa Siku Ya Qiyaamah Kwa Mwenye Kufanya ‘Amali Kwa Riyaa
Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
وَالَّذِينَ يُنفِقُونَ أَمْوَالَهُمْ رِئَاءَ النَّاسِ وَلَا يُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَلَا بِالْيَوْمِ الْآخِرِ ۗ وَمَن يَكُنِ الشَّيْطَانُ لَهُ قَرِينًا فَسَاءَ قَرِينًا ﴿٣٨﴾
Na wale wanaotoa mali zao kwa kujionyesha kwa watu na wala hawamwamini Allaah wala Siku ya Mwisho. Na yule ambaye shaytwaan amekuwa ni rafiki yake mwandani, basi mbaya alioje rafiki mwandani (huyo). [An-Nisaa: 38]
Mafunzo:
Maonyo ya kufanya ‘amali kwa riyaa (kujionyesha): Jundub bin ‘Abdillaah bin Sufyaan (رضي الله عنه) amehadithia kwamba: “Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema:
“Mwenye kuzungumza (au kusoma) ili watu wamsifu, Allaah Atamfedhehesha Siku ya Qiyaamah, na mwenye kuwafanyia watu riyaa (kwa amali njema ili aonekane ni mtukufu), Allaah Atazidhihirisha siri zake (Siku ya Qiyaamah).” [Al-Bukhaariy na Muslim]