036-Aayah Na Mafunzo: Haki Ya Allaah Kwa Waja Wake Na Haki Ya Waja Kwa Allaah

 

Aayah Na Mafunzo

An-Nisaa

Haki Ya Allaah Kwa Waja Wake Na Haki Ya Waja Kwa Allaah

Alhidaaya.com

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَاعْبُدُوا اللَّـهَ وَلَا تُشْرِكُوا بِهِ شَيْئًا ۖ وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًا وَبِذِي الْقُرْبَىٰ وَالْيَتَامَىٰ وَالْمَسَاكِينِ وَالْجَارِ ذِي الْقُرْبَىٰ وَالْجَارِ الْجُنُبِ وَالصَّاحِبِ بِالْجَنبِ وَابْنِ السَّبِيلِ وَمَا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُمْ ۗ إِنَّ اللَّـهَ لَا يُحِبُّ مَن كَانَ مُخْتَالًا فَخُورًا ﴿٣٦﴾

Na mwabuduni Allaah na wala msimshirikishe na chochote. Na wafanyieni ihsaan wazazi wawili na jamaa wa karibu, na mayatima, na masikini na jirani mwenye ujamaa na jirani asiye na ujamaa na rafiki wa karibu, na msafiri aliyeishiwa masurufu, na wale iliyowamiliki mikono yenu ya kulia. Hakika Allaah Hapendi mwenye majivuno mwenye kujifakharisha. [An-Nisaa: 36]

 

 

Mafunzo:

 

Allaah Anaghufuria dhambi zote isipokuwa shirki. Na Mu’aadh bin Jabal (رضي الله عنه) amehadithia kwamba: Nilikuwa nyuma ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) juu ya punda akasema: “Ee Mu’aadh! Unajua nini haki ya Allaah juu ya waja Wake, na nini haki ya waja juu ya Allaah?” Nikajibu: Allaah na Rasuli Wake wanajua zaidi: Akasema: “Haki ya Allaah kwa waja wake ni kwamba wamwabudu na wasimshirikishe na chochote. Na haki ya waja kwa Allaah ni kwamba Hatomwadhibu yeyote ambaye hamshirikishi na chochote.” Nikasema: Ee Rasuli wa Allaah! Niwabashirie watu? Akasema: “Usiwabashirie wasije kuitegemea.” (wakaacha kufanya juhudi katika ‘ibaadah) [Al-Bukhaariy na Muslim].

 

 

 

Share