046-Aayah Na Mafunzo: Mayahudi Na Ahlul-Bid’ah Kupotosha Maana Ya Maneno Ya Qur-aan
Aayah Na Mafunzo
An-Nisaa
Mayahudi Na Ahlul-Bid’ah Kupotosha Maana Ya Maneno Ya Qur-aan
Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
مِّنَ الَّذِينَ هَادُوا يُحَرِّفُونَ الْكَلِمَ عَن مَّوَاضِعِهِ وَيَقُولُونَ سَمِعْنَا وَعَصَيْنَا وَاسْمَعْ غَيْرَ مُسْمَعٍ وَرَاعِنَا لَيًّا بِأَلْسِنَتِهِمْ وَطَعْنًا فِي الدِّينِ ۚ وَلَوْ أَنَّهُمْ قَالُوا سَمِعْنَا وَأَطَعْنَا وَاسْمَعْ وَانظُرْنَا لَكَانَ خَيْرًا لَّهُمْ وَأَقْوَمَ وَلَـٰكِن لَّعَنَهُمُ اللَّـهُ بِكُفْرِهِمْ فَلَا يُؤْمِنُونَ إِلَّا قَلِيلًا ﴿٤٦﴾
Katika Mayahudi wako wanaobadilisha maneno kuyatoa mahali pake, na husema: “Tumesikia” na “Tumeasi”; na (wanamwambia Rasuli): “Sikia bila ya kusikilizwa.” Na (husema): “raa’inaa” kwa kuzipotoa ndimi zao na kutukana Dini. Na lau wangesema: “Tumesikia na tumetii na sikia na “undhwurnaa” ingelikuwa khayr kwao na yenye kufaa zaidi. Lakini Allaah Amewalaani kwa kufru yao; basi hawaamini isipokuwa wachache tu. [An-Nisaa: 46]
Mafunzo:
Miongoni mwa ada za Mayahudi ni kuyapotosha maneno ya Allaah (عزّ وجلّ) kuyatoa kwenye makusudio yake na pia wanayatafsiri kwa isiyokuwa tafsiri yake. Na watu wa bid’ah wamejifananisha nao katika kupindisha na kupotosha maana ya Majina ya Allaah na Sifa Zake.