057-Aayah Na Mafunzo: Jannah Kuna Mti Wenye Kivuli Cha Msafara Wa Miaka Mia Moja
Aayah Na Mafunzo
An-Nisaa
Jannah Kuna Mti Wenye Kivuli Cha Msafara Wa Miaka Mia Moja
Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
وَالَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ سَنُدْخِلُهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا ۖ لَّهُمْ فِيهَا أَزْوَاجٌ مُّطَهَّرَةٌ ۖ وَنُدْخِلُهُمْ ظِلًّا ظَلِيلًا ﴿٥٧﴾
Na wale walioamini na wakatenda mema Tutawaingiza Jannaat zipitazo chini yake mito, ni wenye kudumu humo abadi. Watapata humo wake waliotakasika na Tutawaingiza katika vivuli vya kina. [An-Nisaa: 57]
Mafunzo:
Anas bin Maalik (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hakika Jannah kuna mti, anatembea mwenye kipando chini ya kivuli chake miaka mia moja hakimalizi.” [Al-Bukhaariy].