048-Aayah Na Mafunzo: Allaah Hamghufurii Mja Atakayefariki Bila Ya Kutubia Katika Kumshirikisha
Aayah Na Mafunzo
An-Nisaa
Allaah Hamghufurii Mja Atakayefariki Bila Ya Kutubia Katika Kumshirikisha
Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
إِنَّ اللَّـهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ ۚ وَمَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَقَدِ افْتَرَىٰ إِثْمًا عَظِيمًا ﴿٤٨﴾
Hakika Allaah Haghufurii kushirikishwa; lakini Anaghufuria yasiyokuwa hayo kwa Amtakae. Na yeyote atakayemshirikisha Allaah basi kwa yakini amezua dhambi kuu.
Mafunzo:
Shirki ni dhambi kubwa ambayo Allaah (سبحانه وتعالى) Hamghufurii mja wake ikiwa hajatubia kabla ya kufariki kwake. Makemeo mazito yametajwa katika Qur-aan na Sunnah, miongoni mwayo ni Hadiyth zifuatazo:
عن ابن مسعود رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((مَنْ مَاتَ يُشْرِكُ بِاللَّهِ شَيْئًا دَخَلَ النَّارَ))
Kutoka kwa Ibn Mas‘uwd pia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Atakayefariki akiwa katika hali ya kumshirikisha Allaah kwa chochote ataingia Motoni)) [Al-Bukhaariy 1238, Muslim 92]
Na pia,
عَن عبدالله بن عمر جاءَ أعرابيٌّ إلى النَّبيِّ صلَّى اللَّهُ عليْهِ وسلَّمَ فقالَ: يا رسولَ اللَّهِ إنَّ أبي كانَ يصِلُ الرَّحمَ وَكانَ وَكانَ فأينَ هوَ؟ قالَ: ((في النَّارِ)) قالَ فَكأنَّهُ وجدَ من ذلِكَ فقالَ: يا رسولَ اللَّهِ فأينَ أبوكَ قالَ رسولُ اللَّهِ صلَّى اللَّهُ عليْهِ وسلَّمَ: ((حيثُما مررتَ بقبرِ مشرِكٍ فبشِّرْهُ بالنَّارِ)) قالَ: فأسلمَ الأعرابيُّ بعدُ وقالَ: لقد كلَّفني رسولُ اللَّهِ صلَّى اللَّهُ عليْهِ وسلَّمَ تعبًا ما مررتُ بقبرِ كافرٍ إلَّا بشَّرتُهُ بالنَّارِ
‘Abdullaah bin ‘Umar (رضي الله عنه) amehadithia: Bedui mmoja alikuwa kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Ee Rasuli wa Allaah! Baba yangu alikuwa akiunga undugu na alikuwa akifanya kadhaa wa kadhaa, je, yuko wapi? Akasema: “Motoni.” Ikawa kama kwamba lilikuwa jambo zito kwake. Akasema: Ee Rasuli wa Allaah! Je, kwani baba yako yuko wapi? Akasema: “Utakapopita kaburi la mushrik yeyote mbashirie moto.” Bedui akasilimu baada ya hapo kisha akasema: Hakika Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم): amenitwika jukumu gumu kwamba kila nikipata kaburi la kafiri nimbashirie moto.” [Swahiyh Ibn Maajah 1288].
Bonyeza kiungo kifuatacho upate faida ziyada: