080-Aayah Na Mafunzo: Kumtii Rasuli Ni Kumtii Allaah Na Kumuasi Ni Kumuasi Allaah
Aayah Na Mafunzo
An-Nisaa
Kumtii Rasuli Ni Kumtii Allaah Na Kumuasi Ni Kumuasi Allaah
Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
مَّن يُطِعِ الرَّسُولَ فَقَدْ أَطَاعَ اللَّـهَ ۖ وَمَن تَوَلَّىٰ فَمَا أَرْسَلْنَاكَ عَلَيْهِمْ حَفِيظًا ﴿٨٠﴾
Atakayemtii Rasuli basi kwa yakini amemtii Allaah. Na atakayekengeuka basi Hatukukutuma kuwa mlinzi juu yao. [An-Nisaa: 80]
Mafunzo:
عَنْ أبي هُرَيْرة رضى الله عنه أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ " مَنْ أَطَاعَنِي فَقَدْ أَطَاعَ اللَّهَ، وَمَنْ عَصَانِي فَقَدْ عَصَى اللَّهَ، وَمَنْ أَطَاعَ أَمِيرِي فَقَدْ أَطَاعَنِي، وَمَنْ عَصَى أَمِيرِي فَقَدْ عَصَانِي ".
Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) amehadithia kuwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Atakayenitii basi atakuwa amemtii Allaah, na atakayeniasi atakuwa amemuasi Allaah, na atakayemtii Amiri wangu (kiongozi niliyemteua), atakuwa amenitii mimi na atakayemuasi atakuwa ameniasi mimi.” [Al-Bukhaariy, Muslim, An-Nasaaiy, Ibn Maajah]
Na pia,
عَنْ أَبي هريرةَ رضي الله عنه: أنَّ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((كُلُّ أُمَّتِي يَدخُلُونَ الجَنَّةَ إلا مَنْ أبَى)). قيلَ: وَمَنْ يَأبَى يَا رَسُول الله؟ قَالَ: ((مَنْ أَطَاعَنِي دَخَلَ الجَنَّةَ، وَمَنْ عَصَانِي فَقَدْ أبَى)). رواه البخاري
Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) amesimulia: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Ummah wangu wote wataingia Jannah isipokuwa atakayekataa.” Akaulizwa: Ni yupi atakayekataa Ee Rasuli wa Allaah? Akajibu: “Atakayenitii mimi ataingia Jannah, na atakayeniasi basi amekataa.” [Al-Bukhaariy]