082-Aayah Na Mafunzo: Radd Kwa Mufawwidhwah Wanaodai Kuwa Sifa Za Allaah Haifahamiki
Aayah Na Mafunzo
An-Nisaa
Radd Kwa Mufawwidhwah Wanaodai Kuwa Sifa Za Allaah Haifahamiki
Alhidaaya.com
Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
أَفَلَا يَتَدَبَّرُونَ الْقُرْآنَ ۚ وَلَوْ كَانَ مِنْ عِندِ غَيْرِ اللَّـهِ لَوَجَدُوا فِيهِ اخْتِلَافًا كَثِيرًا ﴿٨٢﴾
Je, hawaizingatii Qur-aan? Na lau ingelikuwa imetoka kwa ghairi ya Allaah, bila shaka wangelikuta ndani yake khitilafu nyingi. [An-Nisaa: 82]
Mafunzo:
Aayah hii ni miongoni mwa dalili na radd juu ya madh-hab ya Al-Mufawwidhwah (wanaokubali sifa ya Allaah lakini wakidai maana yake haijulikani; kwa hivyo, wanamzulia Allaah kuwa kawaletea mafundisho waja Wake ambayo hayajulikani maana yake!) ambao wanasema kuwa Majina ya Allaah na Swifaat Zake hazifahamiki maana yake, na hiyo ni itikadi batili mno, bali Shaykhul-Islaam (رحمه الله) amesema alipolizungumzia hili pote la Mufawwidhwah kuwa ni katika mapote ya bid’ah yaliyokuwa ya shari. Kisha wakainasibisha kauli hii kuwa ndiyo kauli ya Salaf! Huko ni kuwazulia wema waliotangulia (رحمهم الله). Imaam Ahmad anawaona Mufawwidhwah kuwa ni wabaya zaidi kuliko Jahmiyyah.