142-Aayah Na Mafunzo: Anayemshirikisha Allaah Kwa Riyaa Hatoipokea 'Amali Yake
Aayah Na Mafunzo
An-Nisaa
Anayemshirikisha Allaah Kwa Riyaa Hatoipokea 'Amali Yake
إِنَّ الْمُنَافِقِينَ يُخَادِعُونَ اللَّـهَ وَهُوَ خَادِعُهُمْ وَإِذَا قَامُوا إِلَى الصَّلَاةِ قَامُوا كُسَالَىٰ يُرَاءُونَ النَّاسَ وَلَا يَذْكُرُونَ اللَّـهَ إِلَّا قَلِيلًا ﴿١٤٢﴾
142. Hakika wanafiki (wanadhani) wanamhadaa Allaah, na hali Yeye (Allaah) Ndiye Mwenye kuwahadaa. Na wanaposimama kuswali husimama kwa uvivu, wakijionyesha kwa watu na wala hawamdhukuru Allaah isipokuwa kidogo tu.
Mafunzo:
Matahadharisho ya riyaa: Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) ameahadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Allaah (تعالى) Anasema: ‘‘Mimi ni Mwenye kujitosheleza kabisa, Sihitaji msaada wala mshirika. Kwa hiyo, yule afanyaye ‘amali kwa kunishirikisha na mtu, Nitaikanusha pamoja na mshirika wake.” Yaani: hatopata ujira wowote kwa ‘amali hiyo. [Muslim (2985), Ibn Maajah (4202)].
Aksema pia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم):
“
Mwenye kuzungumza (au kusoma) ili watu wamsifu, Allaah Atamfedhehesha Siku ya Qiyaamah, na mwenye kuwafanyia watu riyaa (kwa amali njema ili aonekane ni mtukufu), Allaah Atazidhihirisha siri zake (Siku ya Qiyaamah).” [Al-Bukhaariy na Muslim]