164-Aayah Na Mafunzo: Swiffah Ya Al-Kalaam Maneno Imethibiti Kwa Allaah

Aayah Na Mafunzo

An-Nisaa

Swiffah Ya Al-Kalaam Maneno Imethibiti Kwa Allaah

 

 

 

 

 

وَرُسُلًا قَدْ قَصَصْنَاهُمْ عَلَيْكَ مِن قَبْلُ وَرُسُلًا لَّمْ نَقْصُصْهُمْ عَلَيْكَ ۚ وَكَلَّمَ اللَّـهُ مُوسَىٰ تَكْلِيمًا ﴿١٦٤﴾

 Na Rusuli Tuliokwishakusimulia kabla, na Rusuli (wengine) Hatukukusimulia. Na bila shaka Allaah Alimsemesha Muwsaa maneno moja kwa moja. [An-Nisaa: (5:164)]

 

Mafunzo:

 

Aqiydah Ya Ahlus-Sunnah Wal-Jamaa’ah Kuhusiana Na Majina Mazuri Kabisa Ya Allaah (سبحانه وتعالى) Na Sifa Zake:

 

Allaah (سبحانه وتعالى)  Alimsemesha Muwsaa (عليه السلام)  Maneno kwa uhakika wake na si kwa majazi kama wanavyosema watu wa bid’ah,  bali ni maneno yaliyojengeka kwa herufi na sauti. Na Sifa ya Maneno ni Sifa iliyothibiti kwa Allaah kwa uhakika wake bila kuifanyia Ta'twiyl (kuzipinga, kukanusha uwezekano), wala Tamthiyl (kumithilisha, kufafanisha, kulinganisha), wala Takyiyf (kuainisha maana na kuziulizia namna yake au kuuliza ni vipi Sifa hiyo ipo, kuchunguza ni kwa “namna gani” zimefungamana au kuambatana na Allaah), wala Tahriyf (kubadilisha maana, kupotosha Sifa ya Allaah (سبحانه وتعالى) kwa kutoa maana isiyo sahihi).

 

Na hii ndiyo kauli ya sawa ambayo wamepita kwayo Salaf na Maimamu wa haki katika Uislamu katika Sifa Zote zilizokuja ndani ya Qur-aan na Sunnah.  

 

 

 

Share