011-Asbaabun-Nuzuwl: An-Nisaa Aayah 011: يُوصِيكُمُ اللَّـهُ فِي أَوْلَادِكُمْ ۖ لِلذَّكَرِ مِثْلُ حَظِّ الْأُنثَيَيْنِ
أسْبابُ النُّزُول
Asbaabun-Nuzuwl
Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Aayaat Za Qur-aan)
Imekusanywa na: Alhidaaya.com
An-Nisaa 011-Allaah Anakuamrisheni kuhusu watoto wenu. Mwanamume atastahiki
يُوصِيكُمُ اللَّـهُ فِي أَوْلَادِكُمْ ۖ لِلذَّكَرِ مِثْلُ حَظِّ الْأُنثَيَيْنِ ۚ فَإِن كُنَّ نِسَاءً فَوْقَ اثْنَتَيْنِ فَلَهُنَّ ثُلُثَا مَا تَرَكَ ۖ وَإِن كَانَتْ وَاحِدَةً فَلَهَا النِّصْفُ ۚ وَلِأَبَوَيْهِ لِكُلِّ وَاحِدٍ مِّنْهُمَا السُّدُسُ مِمَّا تَرَكَ إِن كَانَ لَهُ وَلَدٌ ۚ فَإِن لَّمْ يَكُن لَّهُ وَلَدٌ وَوَرِثَهُ أَبَوَاهُ فَلِأُمِّهِ الثُّلُثُ ۚ فَإِن كَانَ لَهُ إِخْوَةٌ فَلِأُمِّهِ السُّدُسُ ۚ مِن بَعْدِ وَصِيَّةٍ يُوصِي بِهَا أَوْ دَيْنٍ ۗ آبَاؤُكُمْ وَأَبْنَاؤُكُمْ لَا تَدْرُونَ أَيُّهُمْ أَقْرَبُ لَكُمْ نَفْعًا ۚ فَرِيضَةً مِّنَ اللَّـهِ ۗ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَلِيمًا حَكِيمًا ﴿١١﴾
11. Allaah Anakuamrisheni kuhusu watoto wenu. Mwanamume atastahiki mfano wa fungu la wanawake wawili. Na ikiwa wanawake ni zaidi ya wawili basi watastahiki theluthi mbili za alichoacha (maiti). Lakini akiwa mtoto wa kike ni mmoja pekee basi atastahiki nusu, na wazazi wake wawili kila mmoja wao atastahiki sudusi katika alichoacha ikiwa anaye mtoto. Na ikiwa hakuwa na mtoto na wazazi wake wawili ndio warithi wake, basi mama yake atastahiki theluthi moja. Na ikiwa anao ndugu basi mama yake atastahiki sudusi, baada ya kutoa wasia aliousia (maiti) au kulipa deni. Baba zenu na watoto wenu hamjui ni yupi miongoni mwao aliye karibu zaidi kwenu kwa manufaa. Ni Shariy’ah kutoka kwa Allaah. Hakika Allaah daima Ni Mjuzi wa yote, Mwenye Hikmah wa yote.
Sababun-Nuzuwl:
Aayah hii pamoja na Aayah ya mwisho katika Suwrah hii (3:176) imeteremka kuhusu Jaabir bin ‘Abdillaah (رضي الله عنه) pale alipotembelewa na Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) akiwa na Abuu Bakr Asw-Swiddiyq (رضي الله عنه) wakamkuta amezimia. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akatawadha na akamrashia maji kutokana na wudhuu wake. Kisha Jaabir (رضي الله عنه) akamuuliza Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم): “Niifanye vipi mali yangu?” Hapo ikateremka Aayah hii. [Amehadithia Jaabir (رضي الله عنه) na imepokelewa na Al-Bukhaariy na Muslim]