022-Asbaabun-Nuzuwl: An-Nisaa Aayah 022: وَلَا تَنكِحُوا مَا نَكَحَ آبَاؤُكُم مِّنَ النِّسَاءِ إِلَّا مَا قَدْ سَلَفَ

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

An-Nisaa     022-Na wala msiwaoe wanawake waliowaoa baba zenu isipokuwa

 

وَلَا تَنكِحُوا مَا نَكَحَ آبَاؤُكُم مِّنَ النِّسَاءِ إِلَّا مَا قَدْ سَلَفَ ۚ إِنَّهُ كَانَ فَاحِشَةً وَمَقْتًا وَسَاءَ سَبِيلًا ﴿٢٢﴾

22. Na wala msiwaoe wanawake waliowaoa baba zenu isipokuwa yaliyokwisha pita. Hakika hayo yalikuwa ni uchafu na chukizo na njia ovu.

 

Sababun-Nuzuwl:

 

Aayah hii imeteremka kwa kuwa watu wa zama za Jaahiliyyah walikuwa wanaharamisha yaliyo ya haramu isipokuwa mke wa baba. Na walikuwa wanakusanya mabinti wawili ambao ni ndugu katika ndoa moja na kwa wakati mmoja, kisha ikateremka Aayah hii pamoja na Kauli ya Allaah Aliposema:

 

  وَأُمَّهَاتُ نِسَائِكُمْ وَرَبَائِبُكُمُ اللَّاتِي فِي حُجُورِكُم مِّن نِّسَائِكُمُ اللَّاتِي دَخَلْتُم بِهِنَّ فَإِن لَّمْ تَكُونُوا دَخَلْتُم بِهِنَّ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ وَحَلَائِلُ أَبْنَائِكُمُ الَّذِينَ مِنْ أَصْلَابِكُمْ وَأَن تَجْمَعُوا بَيْنَ الْأُخْتَيْنِ إِلَّا مَا قَدْ سَلَفَ ۗ

… na mama wa wake zenu, na watoto wenu wa kambo walio katika ulinzi wenu waliozaliwa na wake zenu ambao mmewaingilia. Lakini ikiwa hamkuwaingilia basi hakuna dhambi (kuwaoa). Na (mmeharamishwa) wake wa watoto wenu waliotoka katika migongo yenu, na kuwaoa dada wawili kwa wakati mmoja, isipokuwa yaliyokwisha pita. [An-Nisaa (4:23)] [Amehadithia Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما)  na imetajwa na Ibn Jariyr Atw-Twabariy katika Tafsiyr yake]  

 

 

Share