059-Asbaabun-Nuzuwl: An-Nisaa Aayah 059: يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَطِيعُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَأُولِي الْأَمْرِ مِنكُمْ
أسْبابُ النُّزُول
Asbaabun-Nuzuwl
Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Aayaat Za Qur-aan)
Imekusanywa na: Alhidaaya.com
An-Nisaa 059- Enyi walioamini! Mtiini Allaah na mtiini Rasuli na wenye madaraka...
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَطِيعُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَأُولِي الْأَمْرِ مِنكُمْ ۖ فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّـهِ وَالرَّسُولِ إِن كُنتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۚ ذَٰلِكَ خَيْرٌ وَأَحْسَنُ تَأْوِيلًا ﴿٥٩﴾
59. Enyi walioamini! Mtiini Allaah na mtiini Rasuli na wenye madaraka katika nyinyi. Mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Allaah na Rasuli mkiwa mnamwamini Allaah na Siku ya Mwisho. Hivyo ni bora na matokeo mazuri zaidi.
Sababun-Nuzuwl:
Aayah hii imeteremka kuhusu ‘Abdullaah Ibn Hudhaafah (رضي الله عنه) pale alipotumwa na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kwenye msafara wa Jihaad. [Amehadithia Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) na imepokelewa na Al-Bukhaariy na Muslim]
Pia Imeteremshwa pale Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alipotuma jeshi chini ya uongozi wa mtu mmoja wa Answaar. Walipoondoka, aliwaghadhibikia kwa sababu fulani akawaambia: Kwani Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) hakukuamrisheni mnitii? Wakasema: Ndio! Akasema: Okoteni kuni. Kisha akawasha moto akasema: Nakuamrisheni muingie motoni humu. Wakakaribia watu kuuingia lakini kijana mmoja miongoni mwao akasema: Nyinyi mmekimbia moto kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) hivyo msikimbilie mpaka mrudi kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kisha akikuamrisheni kuingia hapo muuingie. Waliporudi kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) wakamwelezea yaliyojiri, kisha yeye akasema: “Mngeliuingia, msingetoka kamwe humo. Hakika utiifu ni katika mema.” [Al-Bukhaariy na Muslim]