065-Asbaabun-Nuzuwl: An-Nisaa Aayah 065: فَلَا وَرَبِّكَ لَا يُؤْمِنُونَ حَتَّىٰ يُحَكِّمُوكَ فِيمَا شَجَرَ بَيْنَهُمْ
أسْبابُ النُّزُول
Asbaabun-Nuzuwl
Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Aayaat Za Qur-aan)
Imekusanywa na: Alhidaaya.com
065-Basi mambo si kama wanavyodai. Naapa kwa Rabb wako, hawatakuwa Waumini wa kweli mpaka …
فَلَا وَرَبِّكَ لَا يُؤْمِنُونَ حَتَّىٰ يُحَكِّمُوكَ فِيمَا شَجَرَ بَيْنَهُمْ ثُمَّ لَا يَجِدُوا فِي أَنفُسِهِمْ حَرَجًا مِّمَّا قَضَيْتَ وَيُسَلِّمُوا تَسْلِيمًا ﴿٦٥﴾
Basi mambo si kama wanavyodai. Naapa kwa Rabb wako, hawatakuwa Waumini wa kweli mpaka wakufanye wewe ni mwamuzi katika yale wanayozozana baina yao, kisha wasipate katika nyoyo zao ukakasi katika yale uliyohukumu na waikubali hukmu yako kwa moyo safi na maridhio [An-Nisaa: 65]
Sababun-Nuzuwl:

Aayah hii imeteremka kuhusu Az-Zubayr bin Al-‘Awwaam (رضي الله عنه) na bwana mmoja katika Answaar, pale walipokhitilafiana kuhusu mfereji wa kupitisha maji ya mvua waliokuwa wakitumia maji yake. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akatoa hukmu baina yao kwamba Az-Zubayr amwagilie maji ardhini mwake kisha ayaache yatiririke kwa Answaar. Akakasirika Answaar huyo na kumwambia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): “Umempendelea yeye kwa kuwa ni mtoto wa ‘ammat yako! Hapo Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akabadilika uso rangi kwa hasira na akamwambia tena Az-Zubayr amwagie maji kwanza kisha ayaachie yatiririke kwa jirani yake huyo kwa kuwa hukumu hiyo ilikuwa kwa manufaa ya wote wawili. Hivyo akampatia Az-Zubayr haki yake. Ikateremka Aayah hii:
فَلَا وَرَبِّكَ لَا يُؤْمِنُونَ حَتَّىٰ يُحَكِّمُوكَ فِيمَا شَجَرَ بَيْنَهُمْ ثُمَّ لَا يَجِدُوا فِي أَنفُسِهِمْ حَرَجًا مِّمَّا قَضَيْتَ وَيُسَلِّمُوا تَسْلِيمًا ﴿٦٥﴾
Basi mambo si kama wanavyodai. Naapa kwa Rabb wako, hawatakuwa Waumini wa kweli mpaka wakufanye wewe ni mwamuzi katika yale wanayozozana baina yao, kisha wasipate katika nyoyo zao ukakasi katika yale uliyohukumu na waikubali hukmu yako kwa moyo safi na maridhio [An-Nisaa: 65]
[Amehadithia Az-Zubayr (رضي الله عنه) na imepokelewa na Al-Bukhaariy na Muslim]