069-Asbaabun-Nuzuwl: An-Nisaa Aayah 069: وَمَن يُطِعِ اللَّـهَ وَالرَّسُولَ فَأُولَـٰئِكَ مَعَ الَّذِينَ أَنْعَمَ اللَّـهُ عَلَيْهِم مِّنَ النَّبِيِّينَ
أسْبابُ النُّزُول
Asbaabun-Nuzuwl
Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Aayaat Za Qur-aan)
Imekusanywa na: Alhidaaya.com
An-Nisaa 069-Na atakayemtii Allaah na Rasuli, basi hao watakuwa pamoja...
وَمَن يُطِعِ اللَّـهَ وَالرَّسُولَ فَأُولَـٰئِكَ مَعَ الَّذِينَ أَنْعَمَ اللَّـهُ عَلَيْهِم مِّنَ النَّبِيِّينَ وَالصِّدِّيقِينَ وَالشُّهَدَاءِ وَالصَّالِحِينَ ۚ وَحَسُنَ أُولَـٰئِكَ رَفِيقًا ﴿٦٩﴾
69. Na atakayemtii Allaah na Rasuli, basi hao watakuwa pamoja na wale Allaah Aliowaneemesha miongoni mwa Manabii na Swiddiqiyna na Mashuhadaa na Swalihina, na uzuri ulioje kuwa pamoja na hao
Sababun-Nuzuwl:
Aayah hii imeteremka kuhusu Answaar mmoja ambaye alikuwa kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akiwa na huzuni. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akamuuliza: “Mbona nakuona umehuzunika?” Akasema: Ee Rasuli wa Allaah! Nilikuwa natafakari jambo. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Jambo gani?” Akajibu: Kila siku tunakuja kwako asubuhi na usiku tukitazama uso wako na kukaa kitako nawe. Lakini kesho (Aakhirah), utakuja kufufuliwa pamoja na Manabii na hivyo sisi hatutoweza kukuona tena. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) hakusema kitu, kisha Jibriyl (عليه السلام) akamjia kumteremshia Aayah hii:
وَمَن يُطِعِ اللَّـهَ وَالرَّسُولَ فَأُولَـٰئِكَ مَعَ الَّذِينَ أَنْعَمَ اللَّـهُ عَلَيْهِم مِّنَ النَّبِيِّينَ وَالصِّدِّيقِينَ وَالشُّهَدَاءِ وَالصَّالِحِينَ ۚ وَحَسُنَ أُولَـٰئِكَ رَفِيقًا ﴿٦٩﴾
Na atakayemtii Allaah na Rasuli, basi hao watakuwa pamoja na wale Allaah Aliowaneemesha miongoni mwa Manabii na Swiddiqiyna na Mashuhadaa na Swalihina, na uzuri ulioje kuwa pamoja na hao! (4:69)
[Ibn Jariyr, Tafsiyr Ibn Kathiyr]
Sababun-Nuzuwl:
Pia Sababun-Nuzuwl ya Aayah hii, ni kama alivyohadithia Mama wa Waumini ‘Aaishah (رضي الله عنها) kwamba: Mtu mmoja alikuja kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Ee Rasuli wa Allaah! Hakika wewe ni kipenzi kwangu kuliko nafsi yangu, na kipenzi kwangu kuliko ahli yangu, na kipenzi kwangu kuliko wanangu. Na hakika ninapokuwa nyumbani kwangu nakukumbuka, basi huwa siwezi kusubiri mpaka nije kukutazama. Na ninapokumbuka mauti yangu na mauti yako, basi hutambua kwamba wewe utakapoingia Jannah utapanda pamoja na Manabii, lakini nitakapoingia mimi Jannah nakhofu kuwa sitokuona! Basi Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) hakumjibu mpaka hapo ikateremshwa:
وَمَن يُطِعِ اللَّـهَ وَالرَّسُولَ فَأُولَـٰئِكَ مَعَ الَّذِينَ أَنْعَمَ اللَّـهُ عَلَيْهِم مِّنَ النَّبِيِّينَ وَالصِّدِّيقِينَ وَالشُّهَدَاءِ وَالصَّالِحِينَ ۚ وَحَسُنَ أُولَـٰئِكَ رَفِيقًا ﴿٦٩﴾
Na atakayemtii Allaah na Rasuli, basi hao watakuwa pamoja na wale Allaah Aliowaneemesha miongoni mwa Manabii na Swiddiqiyna na Mashuhadaa na Swalihina, na uzuri ulioje kuwa pamoja na hao! (4:69).
[At-Twabaraaniy katika Al-Mu’jamu Asw-Swaghiyr]