128-Asbaabun-Nuzuwl: An-Nisaa Aayah 128: وَإِنِ امْرَأَةٌ خَافَتْ مِن بَعْلِهَا نُشُوزًا أَوْ إِعْرَاضًا فَلَا جُنَاحَ عَلَيْهِمَا أَن يُصْلِحَا بَيْنَهُمَا
أسْبابُ النُّزُول
Asbaabun-Nuzuwl
Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Aayaat Za Qur-aan)
Imekusanywa na: Alhidaaya.com
An-Nisaa 128-Na ikiwa mke atakhofia kutoka kwa mumewe uonevu wa ndoa au kutengwa...
وَإِنِ امْرَأَةٌ خَافَتْ مِن بَعْلِهَا نُشُوزًا أَوْ إِعْرَاضًا فَلَا جُنَاحَ عَلَيْهِمَا أَن يُصْلِحَا بَيْنَهُمَا صُلْحًا ۚ وَالصُّلْحُ خَيْرٌ ۗ وَأُحْضِرَتِ الْأَنفُسُ الشُّحَّ ۚ وَإِن تُحْسِنُوا وَتَتَّقُوا فَإِنَّ اللَّـهَ كَانَ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرًا ﴿١٢٨﴾
Na ikiwa mke atakhofia kutoka kwa mumewe uonevu wa ndoa au kutengwa, basi si vibaya kwao wawili wakisikilizana baina yao kwa suluhu. Na suluhu ni bora zaidi. Na nafsi zimeumbiwa tabia ya uchoyo na ubahili. Na mkifanya ihsaan (kwa wanawake) na mkawa na taqwa, basi hakika Allaah kwa yale myatendayo Ni Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika. (4:128).
Sababun-Nuzuwl:
Aayah hii imeteremshwa kuhusu bwana mmoja aliyekuwa na mke lakini hakuwa akimuonyesha mahaba wala hamkithirishii katika mahaba na wala hamuonyeshi mwenendo uliokuwa mzuri. Huyo bwana hakutaka kuendelea (naye katika ndoa), na alishazaa naye mtoto, lakini huyo mke hakupenda apewe talaka. Basi akamwambia mumewe: “Nakuruhusu uishi na mke mwengine.” [Al-Bukhaariy na Muslim].
Katika riwaaya nyengine mwanamke huyo alisema: “Naachilia mbali haki zangu, lakini usinitaliki.” Hapo ikateremka Aayah hii: