176-Asbaabun-Nuzuwl: An-Nisaa Aayah 176: يَسْتَفْتُونَكَ قُلِ اللَّـهُ يُفْتِيكُمْ فِي الْكَلَالَةِ
أسْبابُ النُّزُول
Asbaabun-Nuzuwl
Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Aayaat Za Qur-aan)
Imekusanywa na: Alhidaaya.com
An-Nisaa 176-Wanakuuliza hukmu ya kishariy’ah. Sema: Allaah Anakubainishieni kuhusu Al-Kalaalah...
يَسْتَفْتُونَكَ قُلِ اللَّـهُ يُفْتِيكُمْ فِي الْكَلَالَةِ ۚ إِنِ امْرُؤٌ هَلَكَ لَيْسَ لَهُ وَلَدٌ وَلَهُ أُخْتٌ فَلَهَا نِصْفُ مَا تَرَكَ ۚ وَهُوَ يَرِثُهَا إِن لَّمْ يَكُن لَّهَا وَلَدٌ ۚ فَإِن كَانَتَا اثْنَتَيْنِ فَلَهُمَا الثُّلُثَانِ مِمَّا تَرَكَ ۚ وَإِن كَانُوا إِخْوَةً رِّجَالًا وَنِسَاءً فَلِلذَّكَرِ مِثْلُ حَظِّ الْأُنثَيَيْنِ ۗ يُبَيِّنُ اللَّـهُ لَكُمْ أَن تَضِلُّوا ۗ وَاللَّـهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ ﴿١٧٦﴾
Wanakuuliza hukmu ya kishariy’ah. Sema: Allaah Anakubainishieni kuhusu Al-Kalaalah (asiye na wazazi wala watoto) Ikiwa mtu amefariki hana mtoto lakini ana dada; basi atastahiki nusu ya yale aliyoyaacha. Na yeye (huyo mtu) atamrithi huyo dada kama hana mtoto. Na ikiwa madada ni wawili; basi watastahiki thuluthi mbili ya yale aliyoyaacha (maiti). Na wakiwa ni ndugu wanaume na wanawake, basi mwanamme atastahiki sehemu iliyo sawa na sehemu ya wanawake wawili. Allaah Anakubainishieni ili msipotee; na Allaah kwa kila kitu ni Mjuzi. (4:176).
Sababun-Nuzuwl:
Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alipomtembelea Jaabir (رضي الله عنه) alipokuwa mgonjwa, Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alimkuta Jaabir akiwa amezimia. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akatawadha na akamrashia maji ya wudhuu, Jaabir akazindukana. Kisha Jaabir akamuuliza Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) namna gani ataigawa mali yake kwa sababu hali yake ni hali ya Al-Kalaalah (asiye na watoto, wala wazazi. Au asiye na mrithi wa kwenda juu wala kwenda chini) na hapo ikateremka Aayah hii:
يَسْتَفْتُونَكَ قُلِ اللَّـهُ يُفْتِيكُمْ فِي الْكَلَالَةِ ۚ إِنِ امْرُؤٌ هَلَكَ لَيْسَ لَهُ وَلَدٌ وَلَهُ أُخْتٌ فَلَهَا نِصْفُ مَا تَرَكَ ۚ وَهُوَ يَرِثُهَا إِن لَّمْ يَكُن لَّهَا وَلَدٌ ۚ فَإِن كَانَتَا اثْنَتَيْنِ فَلَهُمَا الثُّلُثَانِ مِمَّا تَرَكَ ۚ وَإِن كَانُوا إِخْوَةً رِّجَالًا وَنِسَاءً فَلِلذَّكَرِ مِثْلُ حَظِّ الْأُنثَيَيْنِ ۗ يُبَيِّنُ اللَّـهُ لَكُمْ أَن تَضِلُّوا ۗ وَاللَّـهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ ﴿١٧٦﴾
Wanakuuliza hukmu ya kishariy’ah. Sema: Allaah Anakubainishieni kuhusu Al-Kalaalah (asiye na wazazi wala watoto) Ikiwa mtu amefariki hana mtoto lakini ana dada; basi atastahiki nusu ya yale aliyoyaacha. Na yeye (huyo mtu) atamrithi huyo dada kama hana mtoto. Na ikiwa madada ni wawili; basi watastahiki thuluthi mbili ya yale aliyoyaacha (maiti). Na wakiwa ni ndugu wanaume na wanawake, basi mwanamme atastahiki sehemu iliyo sawa na sehemu ya wanawake wawili. Allaah Anakubainishieni ili msipotee; na Allaah kwa kila kitu ni Mjuzi. (4:176).
[Amehadithia Jaabir (رضي الله عنه) na imepokelewa na Al-Bukhaariy na Muslim]. Na katika riwaayah ya At-Tirmidhiy, Abuu Daawuwd: “(Jaabir) alikuwa na dada tisa.”