041-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Maaidah Aayah 041: يَا أَيُّهَا الرَّسُولُ لَا يَحْزُنكَ الَّذِينَ يُسَارِعُونَ فِي الْكُفْرِ

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

Al-Maaidah   041- Ee Rasuli, wasikuhuzunishe wale wanaokimbilia kukufuru…

 

 

يَا أَيُّهَا الرَّسُولُ لَا يَحْزُنكَ الَّذِينَ يُسَارِعُونَ فِي الْكُفْرِ مِنَ الَّذِينَ قَالُوا آمَنَّا بِأَفْوَاهِهِمْ وَلَمْ تُؤْمِن قُلُوبُهُمْ ۛ وَمِنَ الَّذِينَ هَادُوا ۛ سَمَّاعُونَ لِلْكَذِبِ سَمَّاعُونَ لِقَوْمٍ آخَرِينَ لَمْ يَأْتُوكَ ۖ يُحَرِّفُونَ الْكَلِمَ مِن بَعْدِ مَوَاضِعِهِ ۖ يَقُولُونَ إِنْ أُوتِيتُمْ هَـٰذَا فَخُذُوهُ وَإِن لَّمْ تُؤْتَوْهُ فَاحْذَرُوا ۚ وَمَن يُرِدِ اللَّـهُ فِتْنَتَهُ فَلَن تَمْلِكَ لَهُ مِنَ اللَّـهِ شَيْئًا ۚ أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ لَمْ يُرِدِ اللَّـهُ أَن يُطَهِّرَ قُلُوبَهُمْ ۚ لَهُمْ فِي الدُّنْيَا خِزْيٌ ۖ وَلَهُمْ فِي الْآخِرَةِ عَذَابٌ عَظِيمٌ ﴿٤١﴾

Ee Rasuli! Wasikuhuzunishe wale wanaokimbilia kukufuru, miongoni mwa wasemao kwa midomo yao: Tumeamini na hali nyoyo zao hazikuamini. Na miongoni mwa Mayahudi wako wanaosikiliza kwa makini kwa ajili ya uongo, wanaosikiliza kwa makini kwa ajili ya watu wengine wasiokufikia. Wanageuza maneno kutoka mahali pake wanasema: Mkipewa haya yachukueni, na msipopewa hayo basi jihadharini! Na yule ambaye Allaah Anataka kumtia mtihanini, hutokuwa na uwezo wowote (kusaidia) kwa ajili yake mbele ya Allaah. Hao ndio ambao Allaah Hakutaka kuzitakasa nyoyo zao. Watapata hizaya duniani na Aakhirah watapata adhabu kuu.

 

سَمَّاعُونَ لِلْكَذِبِ أَكَّالُونَ لِلسُّحْتِ ۚ فَإِن جَاءُوكَ فَاحْكُم بَيْنَهُمْ أَوْ أَعْرِضْ عَنْهُمْ ۖ وَإِن تُعْرِضْ عَنْهُمْ فَلَن يَضُرُّوكَ شَيْئًا ۖ وَإِنْ حَكَمْتَ فَاحْكُم بَيْنَهُم بِالْقِسْطِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الْمُقْسِطِينَ﴿٤٢﴾

 (Hao ni) wenye kusikiliza kwa makini uongo, walaji haramu kwa pupa. Basi wakikujia wahukumu baina yao au wapuuze. Na ukiwapuuza, hawatowe za kukudhuru chochote. Na kama ukihukumu, basi hukumu baina yao kwa uadilifu. Hakika Allaah Anapenda wafanyao uadilifu.

 

 

وَكَيْفَ يُحَكِّمُونَكَ وَعِندَهُمُ التَّوْرَاةُ فِيهَا حُكْمُ اللَّـهِ ثُمَّ يَتَوَلَّوْنَ مِن بَعْدِ ذَٰلِكَ ۚ وَمَا أُولَـٰئِكَ بِالْمُؤْمِنِينَ ﴿٤٣﴾

Na vipi watakufanya wewe kuwa hakimu wao na hali wana Tawraat yenye Hukumu ya Allaah ndani yake, kisha baada ya hayo wanakengeuka? Na hao si wenye kuamini.

 

 

إِنَّا أَنزَلْنَا التَّوْرَاةَ فِيهَا هُدًى وَنُورٌ ۚ يَحْكُمُ بِهَا النَّبِيُّونَ الَّذِينَ أَسْلَمُوا لِلَّذِينَ هَادُوا وَالرَّبَّانِيُّونَ وَالْأَحْبَارُ بِمَا اسْتُحْفِظُوا مِن كِتَابِ اللَّـهِ وَكَانُوا عَلَيْهِ شُهَدَاءَ ۚ فَلَا تَخْشَوُا النَّاسَ وَاخْشَوْنِ وَلَا تَشْتَرُوا بِآيَاتِي ثَمَنًا قَلِيلًا ۚ وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْكَافِرُونَ ﴿٤٤﴾

Hakika Sisi Tumeteremsha Tawraat yenye mwongozo na nuru ambayo Manabii waliojisalimisha kikamilifu (kwa Allaah), pamoja na wanachuoni waswalihina na mafuqahaa weledi, wanawahukumia kwayo Mayahudi. Kwa sababu wao wamebebeshwa jukumu la kutakwa kukilinda na kukihifadhi Kitabu cha Allaah, na wakawa mashahidi juu yake. Basi msiwaogope watu, bali Niogopeni Mimi, na wala msibadilishe Aayaat Zangu kwa thamani ndogo. Na yeyote asiyehukumu kwa yale Aliyoyateremsha Allaah, basi hao ndio makafiri.

 

 

وَكَتَبْنَا عَلَيْهِمْ فِيهَا أَنَّ النَّفْسَ بِالنَّفْسِ وَالْعَيْنَ بِالْعَيْنِ وَالْأَنفَ بِالْأَنفِ وَالْأُذُنَ بِالْأُذُنِ وَالسِّنَّ بِالسِّنِّ وَالْجُرُوحَ قِصَاصٌ ۚ فَمَن تَصَدَّقَ بِهِ فَهُوَ كَفَّارَةٌ لَّهُ ۚ وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ ﴿٤٥﴾

Na Tumewaandikia Shariy’ah humo kwamba nafsi kwa nafsi, na jicho kwa jicho, na pua kwa pua, na sikio kwa sikio, jino kwa jino, na majaraha ni kisasi. Lakini atakayesamehe kwa kutolea swadaqah basi itakuwa ni kafara kwake. Na yeyote asiyehukumu kwa yale Aliyoyateremsha Allaah, basi hao ndio madhalimu.

 

 

وَقَفَّيْنَا عَلَىٰ آثَارِهِم بِعِيسَى ابْنِ مَرْيَمَ مُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ مِنَ التَّوْرَاةِ ۖ وَآتَيْنَاهُ الْإِنجِيلَ فِيهِ هُدًى وَنُورٌ وَمُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ مِنَ التَّوْرَاةِ وَهُدًى وَمَوْعِظَةً لِّلْمُتَّقِينَ ﴿٤٦﴾

Na Tukamfuatishia katika njia yao (Manabii hao), ‘Iysaa mwana wa Maryam akisadikisha yale yaliyoko kabla yake katika Tawraat. Na Tukampa Injiyl yenye mwongozo na nuru ndani yake, inasadikisha yale yaliyokuwa kabla yake katika Tawraat, na Tumeifanya mwongozo na mawaidha kwa wenye taqwa.

 

 

وَلْيَحْكُمْ أَهْلُ الْإِنجِيلِ بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ فِيهِ ۚ وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ ﴿٤٧﴾

Na watu wa Injiyl wahukumu kwa yale Aliyoyateremsha Allaah ndani yake. Na yeyote asiyehukumu kwa yale Aliyoyateremsha Allaah, basi hao ndio mafasiki. (5:41-47)

 

 

Sababun-Nuzuwl:

 

 

Aayah hii na zinazofuatia (5:41-47) zimeteremka kama alivyohadithia Al-Baraa bin ‘Aazib (رضي الله عنه)  kwamba: Myahudi mmoja aliyejaa weusi usoni na aliyepigwa mijeledi alipita kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم). Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akamwita akamuuliza: “Je, hivyo ndivyo mlivyokuta (shari’yah) katika Kitabu chenu kuhusu hadd (adhabu) ya mzinifu?” Wakasema: Ndio. Akamwita mtu mmoja miongoni mwa wanachuoni wao akasema: “Nakuuliza kwa kuapia Jina la Allaah Ambaye Ameteremsha Tawraat kwa Muwsaa; je, hivyo ndivyo mnavyokuta hadd ya mzinifu katika Kitabu chenu?” Akasema: Hapana! Usingeniuliza hilo kwa kuapia Jina la Allaah, nisingelikuelezea. (Ni kweli) Tunaikuta Ar-Rajm (adhabu ya kupigwa mawe mpaka kufa) kama ilivyo shari’yah katika Tawraat lakini jarima imezoeleka kwa watu wetu wenye hadhi tu. Hivyo, tunapomkamata tajiri (aliyezini) tunamuachia (huru), lakini tukimkamata aliye duni tunamsimamishia adhabu ya hadd. Kisha tukasema: Njooni tukubaliane (adhabu) tutakayoisimamisha kwa wote, matajiri na walio duni. Hivyo tukaamua kumpaka (mzinifu) masinzi usoni na kumpiga mijeledi badala ya rajm. Hapo Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Ee Allaah, hakika mimi wa kwanza kuihuisha Amri Yako wakati wao (Mayahudi) wameifisha. Basi akaamrisha, na (mkhalifu huyo) akasimamishiwa rajm. Hapo Allaah (سبحانه وتعالى) Akateremsha:

 

يَا أَيُّهَا الرَّسُولُ لَا يَحْزُنكَ الَّذِينَ يُسَارِعُونَ فِي الْكُفْرِ مِنَ الَّذِينَ قَالُوا آمَنَّا بِأَفْوَاهِهِمْ وَلَمْ تُؤْمِن قُلُوبُهُمْ ۛ وَمِنَ الَّذِينَ هَادُوا ۛ سَمَّاعُونَ لِلْكَذِبِ سَمَّاعُونَ لِقَوْمٍ آخَرِينَ لَمْ يَأْتُوكَ ۖ يُحَرِّفُونَ الْكَلِمَ مِن بَعْدِ مَوَاضِعِهِ ۖ يَقُولُونَ إِنْ أُوتِيتُمْ هَـٰذَا فَخُذُوهُ  

Ee Rasuli! Wasikuhuzunishe wale wanaokimbilia kukufuru, miongoni mwa wasemao kwa midomo yao: Tumeamini na hali nyoyo zao hazikuamini. Na miongoni mwa Mayahudi wako wanaosikiliza kwa makini kwa ajili ya uongo, wanaosikiliza kwa makini kwa ajili ya watu wengine wasiokufikia. Wanageuza maneno kutoka mahali pake wanasema: Mkipewa haya yachukueni.,

 

Ikasemwa na Mayahudi: Nendeni kwa Muhammad, akikuamrisheni kukupakeni masinzi na kupigwa mijeledi basi pokeeni, lakini akikupeni hukumu ya rajm, basi tahadharini (jiepusheni). Hapo Allaah (سبحانه وتعالى) Akateremsha:

 

وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْكَافِرُونَ ﴿٤٤﴾

.Na yeyote asiyehukumu kwa yale Aliyoyateremsha Allaah, basi hao ndio makafiri. (5:44).

 

وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ ﴿٤٥﴾

Na yeyote asiyehukumu kwa yale Aliyoyateremsha Allaah, basi hao ndio madhalimu. (5:45).

 

 

وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ ﴿٤٧﴾

Na yeyote asiyehukumu kwa yale Aliyoyateremsha Allaah, basi hao ndio mafasiki. (5:47).

 

Aayah zote hizo (5:41-47) zimeteremshwa kuwahusu makafiri.

 

 

Share