Imaam Ibn Baaz: Hukmu ya Maandamano Katika Uislamu

Hukmu ya Maandamano Katika Uislamu

 

Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah)

www.alhidaaya.com

 

 

Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) amesema:

 

“Tabia njema ni zile zinazotokana na mwenendo mkuu ambao kupitia humo ukweli utakubaliwa, na matendo maovu yanayotokana na mwenendo wa khatari ambao kwa njia hiyo hautokubaliwa, na unapelekea ukandamizaji, uadui na upiganaji.

 

Ikijumuishwa hili ni lile ambalo baadhi ya watu wanafanya, kama maandamano, ambayo yanasababisha maovu makubwa kwa walinganiaji – kuandamana mitaani kwa makundi na kupiga kelele si katika njia ya kurekebisha jambo wala si katika da’wah.

Njia sahihi (kupinga dhulma au ukandamizaji au maovu) ni kumzuru (kuiongozi kwa kumnasihi) na kuandika lile lililo bora – kushauri viongozi na Mashaykh wa makabila (sehemu zenye makabila) – si kwa vurugu na kuandamana.

 

Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa Makkah kwa miaka kumi na hakupatapo kuandamana au kutembea (mitaani) kwa makundi, wala hakupatapo kuwatishia watu mali zao au nafsi zao.

 

Wala hakuna shaka yoyote kwamba njia hii ina madhara kwa da’wah na walinganiaji – inazuia kuenea (Dini) na inawafanya viongozi na wale waliopo madarakani kufanya lolote wanaloweza ili kuyakataa na kuyazuia (hayo maandamano). Hao (waandamanaji) wanatarajia mema kutokana na kuandamana (kwao), lakini wanaloambulia ni kinyume chake!

 

Ni bora kwa mlinganiaji wa Allaah kuchukua njia ya Rusuli na wafuasi wao, hata (kubaki) kwenye wakati wa dhiki, ni bora kuliko kufanya matendo ambayo yatadhuru, yatazuia au yataipinga da’wah. Na hakuna nguvu wala hila isipokuwa ni kutokana na Allaah”.

 

 

[Majalatul-Buhuwth Al-Islaamiyyah, juz. 38, uk. 210]

 

 

Share