Imaam Ibn Baaz: Hukmu Ya Kuvaa Saa Mkono Wa Kushoto
Hukmu Ya Kuvaa Saa Mkono Wa Kushoto
Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah)
SWALI:
Nini hukmu ya wanaume kuvaa saa mkono wa kushoto?
JIBU:
AlhamduliLLaah.
Inafaa kuvaa saa kulia na kushoto kwani imethibiti kutoka kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwamba alikuwa akivaa pete mara kuliani na mara kushotoni. Na hii ni bainisho la kuruhusika kwa wasaa. Na saa ni kama hivyo tu, akivaa (kwenye mkono wa) kulia au kushoto hakuna ubaya.
Imaam ‘Abdul-‘Aziyz Bin Baaz
[Fataawaa Nuwr ‘Alaa Ad-Darb (3/1560)]