008-Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kuomba Maghfirah Na Tawbah Du'aa Ina Jina Tukufu La Allaah Ambalo Likiombwa Huitikiwa
Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
Kuomba Maghfirah Na Tawbah Du'aa Ambayo Ina
Jina Tukufu La Allaah Ambalo Likiombwa Huitikiwa
إِنِّي أَسْأَلُكَ يَا أَللَّهُ بِأَنَّكَ الْوَاحِدُ الاَحَدُ الصَّمَدُ الَّذِي لَمْ يَلِدْ وَلَمْ يُولَدْ وَلَمْ يَكُنْ لَهُ كُفُوًا أَحَدٌ أَنْ تَغْفِرَ لِي ذُنُوبِي إِنَّكَ أَنْتَ الْغَفُورُ الرَّحِيمُ
Allaahumma inniy as-aluka yaa Allaah, biannakal-Waahidusw-Swamadu ALladhiy lam yalid walam yuwlad walam yakullahu kufuwan ahad, an-Taghfiraliy dhunuwbiy innaka Antal-Ghafuwrur-Rahiym
Hakika mimi nakuomba ee Allaah ya kwamba Wewe ni Mmoja Pekee Mtegemewa kwa haja zote, Ambaye Hakuzaa wala Hakuzaliwa wala Hana anayefanana Naye hata mmoja, Unighufurie madhambi yangu, hakika Wewe ni Mwingi wa Kughufuria Mwenye Kurehemu daima
Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): ((Naapa kwa Ambaye nafsi yangu imo Mikononi Mwake, kwa yakini Ameomba kwa Jina Lake Tukufu kabisa ambalo Anapoombwa kwalo [du’aa] Anaitikia na Anapotakwa kwalo [jambo] Hutoa)) [Hadiyth ya Buraydah bin Al-Haswiyb Al-Aslamiyy kutoka kwa baba yake Radhwiya Allaahu ‘anhumaa – Swahiyh Ibn Maajah (3125) Swahiyh At-Tirmidhy (3475), Swahiyh Abi Daawuwd (1493), Swahiyh At-Targhiyb (1640)]