017-Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kuomba Jannah Na Kuepushwa Na Moto Mara Tatu Asubuhi Na Jioni
Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
Kuomba Jannah Na Kuepushwa Na Moto Mara Tatu Asubuhi Na Jioni
اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ الْجَنَّةَ وَأَسْتَجِيرُ بِكَ مِنَ النَّارِ (ثلاث مرات)
Allaahumma inniy as-alukal-Jannata wa astajiyru bika minan-naari [mara 3]
Ee Allaah, hakika mimi nakuomba Jannah na najikinga Kwako dhidi ya Moto
Inapaswa kusomwa katika Swalaah baada ya Tashahhud kabla ya kutoa salaam.
[At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Ibn Maajah – Swahiyh At-Tirmidhiy (2/319) na lafdhi yake ((Atakayemwomba Allaah Jannah mara tatu [asubuhi na jioni], Jannah itasema: Ee Allaah muingize Jannah, na atakayejilinda kwa Allaah na Moto mara tatu, Moto utasema: Ee Allaah mlinde na Moto))