019-Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Adhabu Ya Moto Kaburi, Shari Za Utajiri Na Umasikini, Fitnah Za Masiyh Ad-Dajjaal
Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
Kinga Ya Fitnah Na Adhabu Za Moto, Kaburi, Shari Za Utajiri Na Umasikini, Masiyh Ad-Dajjaal, Kutakaswa Na Madhambi
اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ فِتْنَةِ النَّارِ وَعَذَابِ النَّارِ وَفِتْنَةِ الْقَبْرِ وَعَذَابِ الْقَبْرِ وَشَرِّ فِتْنَةِ الْغِنَى وَشَرِّ فِتْنَةِ الْفَقْرِ. اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ شَرِّ فِتْنَةِ الْمَسِيحِ الدَّجَّالِ. اللَّهُمَّ اغْسِلْ قَلْبِي بِمَاءِ الثَّلْجِ وَالْبَرَدِ وَنَقِّ قَلْبِي مِنْ الْخَطَايَا كَمَا نَقَّيْتَ الثَّوْبَ الأَبْيَضَ مِنْ الدَّنَسِ. وَبَاعِدْ بَيْنِي وَبَيْنَ خَطَايَايَ كَمَا بَاعَدْتَ بَيْنَ الْمَشْرِقِ وَالْمَغْرِبِ. اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ الْكَسَلِ وَالْمَأْثَمِ وَالْمَغْرَمِ.
Allaahumma inniy a’uwdhu bika min fitnatin-naari wa ‘adhaabin-naari wa fitnatil-qabri, wa adhaabil-qabri, wa sharri fitnatil-ghinaa, wa sharri fitnatil-faqri. Allaahumma inniy a’uwdhu bika min sharri fitnatil-Masiyhid-dajjaal. Allaahummagh-sil qalbiy bimaaith-thalji walbaradi, wanaqqi qalbiy minal-khatwaayaa kamaa naqqaytath-thawbal-abyadhw minad-ddanasi, wa baa’id bayniy wa bayna khatwaayaaya kamaa baa’adta baynal-Mashriqi wal-Maghribi. Allaahumma inniy a’uwdhu bika minal-kasli wal-maa-thami wal-maghrami.
Ee Allaah, hakika mimi najikinga Kwako fitna za Moto na adhabu za Moto, na fitna za kaburi, na adhabu za kaburi, na shari za fitna za utajiri, na shari za fitna za ufakiri. Ee Allaah, hakika mimi najikinga Kwako shari za fitna za Masiyh Ad-Dajjaal. Ee Allaah, Osha moyo wangu kwa theluji na barafu na Takasa moyo wangu madhambi kama Ulivyotakasa nguo nyeupe kutokana na uchafu, na niweke mbali baina yangu na baina ya madhambi kama Ulivyoweka mbali baina ya Mashariki na Magharibi. Ee Allaah, hakika najikinga Kwako uvivu na madhambi na deni.
[Al-Bukhaariy na Muslim]