077-Du'aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kuomba Rahmah Ya Allaah Itakayokutosheleza Usimtegemee Yeyote Ila Allaah
Du'aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):
Kuomba Rahmah Ya Allaah Itakayokutosheleza Usimtegemee Yeyote Ila Allaah
اللَّهُمَّ مَالِكُ الْمُلْكِ، تُؤْتِي الْمُلْكَ مَنْ تَشَاءُ، وَتَنْزِعُ الْمُلْكَ مِمَّنْ تَشَاءُ، وَتُعِزُّ مَنْ تَشَاءُ، وَتُذِلُّ مَنْ تَشَاءُ، بِيَدِكَ الْخَيْرِ إِنَّكَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ، رَحْمَانُ الدُّنْيَا وَالآخِرَةِ، تُعْطِيهُمَا مَنْ تَشَاءُ، وَتَمْنَعُ مِنْهُمَا مَنْ تَشَاءُ، ارْحَمْنِي رَحْمَةً تُغْنِينِي بِهَا عَنْ رَحْمَةِ مَنْ سِوَاكَ
Allaahumma Maalikul-Mulki Tu-til-mulka man Tashaau wa Tanzi’ul-mulka mimman Tashaau, wa Tu’izzu man Tashaau, Biyadikal-khayri Innaka ‘alaa kulli shay-in Qadiyr, Rahmaanud-duniyaa wal-Aakhirah, Tu’twiyhumaa man Tashaau wa Tamna’u minhumaa man Tashaau, Irhamniy Rahamatan tughniyniy bihaa ‘an Rahmatin man siwaaka.
Ee Allaah Mfalme Uliyemiliki ufalme wote, Unampa ufalme Umtakaye, na Unamuondoshea ufalme Umtakaye, na Unamtukuza Umtakaye, na Unamdhalilisha Umtakaye, khayr imo Mkononi Mwako. Hakika Wewe juu ya kila kitu ni Muweza. Mwingi wa rahmah duniani na Aakhirah Mwenye kurehemu, Unampa rahmah mbili hizo Umtakaye na Unamnyima Umtakaye. Nirehemu rahmah itakayonitosheleza kwayo rahmah isiyotoka kwa mwengine isipokuwa Wewe
Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimwambia Mu’aadh (Radhwiya Allaahu 'anhu): ((Je, nikufundishe duaa ambayo ukiiomba basi ikiwa una deni mfano wa mlima wa Uhud, Allaah Atakukidhia. Sema ya Mu’aadh: “Ee Allaah Mfalme Uliyemiliki ufalme wote……[Hadiyth Hasan - Swahiyh At-Targhiyb (1821)]