078-Du'aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kuomba Msamaha, Al-'Aafiyah Duniani Na Aakhirah Kuhifadhiwa Kila Pande
Du’aa Za Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)
Kuomba Msamaha, Al-'Aafiyah Duniani Na Aakhirah
Kuhifadhiwa Kila Pande
اللّهُـمَّ إِنِّـي أسْـأَلُـكَ العَـفْوَ وَالعـافِـيةَ في الدُّنْـيا وَالآخِـرَة، اللّهُـمَّ إِنِّـي أسْـأَلُـكَ العَـفْوَ وَالعـافِـيةَ في ديني وَدُنْـيايَ وَأهْـلي وَمالـي، اللّهُـمَّ اسْتُـرْ عـوْراتي وَآمِـنْ رَوْعاتـي، اللّهُـمَّ احْفَظْـني مِن بَـينِ يَدَيَّ وَمِن خَلْفـي وَعَن يَمـيني وَعَن شِمـالي، وَمِن فَوْقـي، وَأَعـوذُ بِعَظَمَـتِكَ أَن أُغْـتالَ مِن تَحْتـي
Allaahumma inniy as-alukal ‘aafiyah fid-dun-yaa wal Aakhirah. Allaahumma inni as-alukal ‘afwa wal ‘aafiyata fiy Diyniy wa dun-yaaya, wa ahliy, wa maaliy. Allaahumma-stur ‘awraatiy, wa-aamin raw’aatiy. Allaahumma-hfadhwniy min bayni yadayya, wamin khalfiy, wa ‘an yamiyniy, wa ‘an shimaaliy, wamin fawqiy, wa a’uwdhu bi’adhwamatika an ughtaala min tahtiy
Ee Allaah, hakika nakuomba msamaha na Al’-Aafiyah (hifadhi ya kila shari, amani, salama) duniani na Aakhirah. Ee Allaah, hakika nakuomba msamaha na Al’-Aafiyah katika Dini na dunia yangu, na ahli wangu, na mali yangu. Ee Allaah nisitiri aibu zangu na nitulize khofu yangu. Ee Allaah, nihifadhi mbele yangu, na nyuma yangu, na kulia kwangu, na kushoto kwangu, na juu yangu, na najikinga kwa Uadhimu Wako kwa kutekwa chini yangu.
Miongoni mwa duaa alizokuwa akiomba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika nyiradi za asubuhi na jioni.
[Hadiyth ya ‘Abdullaah bin ‘Umar (Radhwiya Allaahu ’anhu) Swahiyh Ibn Maajah (2/332), Swahiyh Abiy Daawuwd (5074)].