11-Imaam Ibn ´Uthaymiyn: Swiyaam Ya Gurupu Kwa Ajili Ya Kushaj-ishana
Swiyaam Ya Gurupu Kwa Ajili Ya Kushaj-ishana
Imaam Ibn ´Uthaymiyn
SWALI:
Ipi hukumu ya Swiyaam ya gurupu, kama kukusanyika gurupu la watu na kukubaliana kufunga swiyaam masiku maalumu kama Jumatatu na Al-Khamiys na hivyo kwa jili ya kusaidizana katika wema na taqwa; kwa kuwa mtu ni dhaifu katika nafsi yake anapata nguvu kwa ndugu zake. Ipi hukumu ya hilo?
JIBU:
Naona kuwa si katika Sunnah na ni aina ya bid´ah, ikiwa watakubaliana hilo. Kwa mfano ikiwa tunakataa Takbiyrah za pamoja au dhikr za pamoja, basi Swawm pia ni ‘ibaadah, haifai kuifunga kwa pamoja.
Lakini ikiwa bila ya makubaliano, basi hakuna neno. Kwa mfano imetokea tumefunga siku ya Jumatatu, hivyo wakasema baadhi yetu kuwaambia wengine: “Waliofunga futari itakuwa kwa fulani na tunakubaliana kufuturu kwake”, hivi hakuna ubaya kwa kuwa si jambo lililopangwa na mkusanyiko wao sio ´ibaadah.
‘Ibaadah kufungwa kwa jamii au pekee ni katika jambo liliomo katika Shariy’ah. Na kwa hili lau kama Allaah Asingetuwekea Shari´yah kuswali jamaa´ah, tusingeliswali jama´ah, ingekuwa kuswali jama´ah ni bid´ah. Lakini Allaah Katuwekea hilo katika Shariy´ah. Hali kadhalika Swawm ya pamoja (kundi) na kukubaliana hilo kabla ni aina ya bid’ah.
Baadhi ya watu wanaweza kuuliza kuhusu Swawm ya Ramadhwaan, je si tunafunga pamoja? Ni kweli, lakini hivyo ndivyo ilivyofaradhishwa. Imefaradhishwa kufunga watu wote katika mwezi huu.
Mimi naona mtu aache hivyo (kufunga kwa gurupu) na mtu awe mwenye kumuomba Allaah (´Azza wa Jalla) na ajihesabu nafsi yake. Na ikiwa mtu hawezi kufanya ´ibaadah ila mpaka apate msaada katika fimbo, yaani mpaka waifanye wengine, azima yake itakuwa dhaifu.