12-Imaam Ibn ‘Uthaymiyn: Mtoto Anawajibika Kufunga Swiyaam?
Mtoto Anawajibika Kufunga Swiyaam?
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
SWALI:
Ipi hukumu Swawm ya mtoto?
JIBU:
Swawm ya mtoto kama tulivyosema, ni mustahab (imependekezwa) na si waajib. Mtoto akifunga, anapewa thawabu; na ikiwa ataacha kufunga, hapati dhambi. Hata hivyo, inatakikana kwa mlezi wake kumuamrisha kufunga ili azowee.
[Fataawaa fiy Ahkaam Asw-Swiyaam, uk. 84]
