05-Shaykh ´Abdul-Muhsin Al-‘Abbaad: Kufanya I´itikaaf Haishurutishwi Kuwa Na Swawm
Kufanya I´itikaaf Haishurutishwi Kuwa Na Swawm
Shaykh ´Abdul-Muhsin Al-‘Abbaad (Hafidhwahu Allaah)
SWALI:
Je, ni sharti mtu ili afanye I´tikaaf awe ana Swawm?
JIBU:
Hapakudhihiri kitu kwangu kuwa ni sharti hilo (la mtu awe katika Swawm) kutokana na kufanya kwake (Nabiy Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) I´tikaaf siku kumi za Shawwaal, haikuthibiti kuwa alifunga. Hakuna kinachoonesha kuwa alifunga.
[Bawaabah Al-Haramayn Ash-Shariyfayn]