03- Imaam Ibn Baaz na Imaam Ibn ‘Uthaymiyn : Je, I’tikaaf Inafaa Ki-Shariy’ah Miezi Mingineyo Isiyokuwa Ramadhwaan
Je, I’tikaaf Inafaa Ki-Shariy’ah Miezi Mingineyo Isiyokuwa Ramadhwaan?
Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) na Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
3. Je, I’tikaaf Inafaa Ki-shariy’ah Miezi Mingineyo Isiyokuwa Ramadhwaan?
Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) amesema:
Inafaa ki-shariy’ah Ramadhwaan na miezi mingineyo na ikiwa pamoja na Swiyaam ni bora zaidi.
[Majmuw’ Al-Fataawaa (15/438)]
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:
Inapasa ki-shariy’ah iwe katika Ramadhwaan pekee, lakini ikiwa mtu atafanya I’tikaaf ghairi ya Ramadhwaan itakuwa inafaa.
[Majmuw’ Al-Fataawaa (20/159-160)]