02- Imaam Ibn Baaz na Imaam Ibn ‘Uthaymiyn : Nini Hukmu Ya I’tikaaf?
Nini Hukmu Ya I’tikaaf?
Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) na Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
2. Nini Hukmu Ya I’tikaaf?
Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) amesema:
I’tikaaf ni Sunnah kwa wanaume na wanawake.
[Majmuw’ Al-Fataawaa (15/442)]
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:
Ni Sunnah ya kutafuta Laylatul-Qadr.
[Majmuw’ Al-Fataawaa (20/156)]
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:
I’tikaaf katika Ramadhwaan ni Sunnah aliyoifanya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika uhai wake, kisha wake zake wakafanya I’tikaaf baada yake. Na Ahlul-‘Ilm (Wanachuoni) kwa ijmaa’ wakasema kuwa ni Sunnah.
[Majmuw’ Al-Fataawa (20/158)]