02-Imaam Al-Albaaniy: Asome Qur-aan Pekee Na Aache ‘Amali Nyengine Kama Kutafuta ‘Ilmu Na Da’wah?
Asome Qur-aan Pekee Na Aache ‘Amali Nyengine Kama Kutafuta ‘Ilmu Na Da’wah?
Imaam Al-Albaaniy (Rahimahu-Allaah)
SWALI: Kutoka Kwa Sakiynah, Bint Muhammad Naaswir Ad-Diyn Al-Albaaniy.
Nimesoma kuwa pindi Ramadhwaan inapoanza baadhi ya ‘Ulamaa wanajishughulisha na kusoma Qur-aan tu, pia hata watu wenye ‘ilmu wanafanya hali kadhalika kujishughulisha na Qur-aan tu na wanaacha hata kutoa Fataawa kwa watu. Je, ni sahihi? Je, nami naweza nikaenda nje mwezi huu kwa ajili ya (kujifunza) Qur-aan na nikaacha kusoma Hadiyth, nisome maana ya Qur-aan, darsa za Qur-aan na mengine zaidi ya hayo?
JIBU:
Jibu lako ee binti wangu, ni kama ulivyohisi na jibu lake ni kama maneno ya Ibn Taymiyyah. Hili la kwanza.
La pili - kuhusisha huku jambo hili, halina asili katika Sunnah - lakini kilichoko katika Sunnah ni kinajulikana kwenye Swahiyh Al-Bukhaariy na Muslim ni kukithirisha sana kusoma Qur-aan katika mwezi wa Ramadhwaan.
Ama kuhusisha tu katika mwezi wa Ramadhwaan kusoma Qur-aan bila 'Ibaadah nyingine kama kutafuta elimu, kufundisha Hadiyth, na kubainisha maana yake, jambo hili halina asili. Kadhalika kunaingia maudhui ya kutoa swadaqah, Zakaah, kuwatendea watu wema nk. Kujishughulisha na kisoma (tu) ni jambo halina asili. Jambo lenye asili ni kukithirisha kusoma.
[Fatwa Hukmu Twalab Al-‘Ilm Fiy Ramadhwaan]