02-Imaam Ibn ‘Uthyamiyn: Kufuturu Tende Kwa Idadi Ya Witr
Kufuturu Tende Kwa Idadi Ya Witr
Imaam Ibn ‘Uthyamiyn (Rahimahu-Allaah)
SWALI:
Nimesikia kwammba mwenye swawm anawajibika pale anapofuturu tende, iwe ni idadi ya witr yaani iwe tano au saba na kadhaalika Je ni waajib?
JIBU:
Si waajib, bali hata sio Sunnah mtu afuturu kwa witr; tatu au tano au saba au tisa isipokuwa Siku ya ‘Iyd kwani imethibiti kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa hatoki kwenda Swalaah Siku ya ‘Iydul-Fitwr mpaka ale kwanza tamar (tende) na alikuwa akila kwa witr.
Ama nje ya hayo Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hakukusudia kula tende kwa witr.
[Fataawa Nuwr ‘Alad-Darb 11/2]