01-Imaam Ibn ‘Uthaymiyn: Israfu Ya Chakula Wakati Wa Futari

Israfu Ya Chakula Wakati Wa Futari

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)

 

 

www.alhidaaya.com

 

  

SWALI:

 

Je, mtu hupata thawabu ndogo (ya Swawm) ikiwa atakithirisha kukata Swawm (Futari) kwa masahani ya vyakula mbali mbali?

 

JIBU:

 

Hapana, hupati thawabu ndogo ya Swawm. Mtu kufanya kitendo cha haraam baada ya kumaliza Swawm, (kitendo kile) hakiathiri thawabu (za Swawm). Bali inaingia katika neno Lake Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):

وَكُلُوا وَاشْرَبُوا وَلَا تُسْرِفُوا ۚ إِنَّهُ لَا يُحِبُّ الْمُسْرِفِينَ ﴿٣١﴾

“Na kuleni na kunyweni; na wala msifanye israfu. Hakika Yeye (Allaah) Hapendi wanaofanya israfu. [Al-A’raaf 7: 31]

 

Huku kufanya israfu ndiyo haraam. Na iktisadi ni nusu ya maisha.  Ikiwa bila kukusudia kutabaki chakula, ni afadhali kitolewe swadaqah.

 

 

[Fiqhu Al-'Ibaadah, uk. 252]

 

 

Share