04-Imaam Ibn ‘Uthaymiyn: Mwanamke Kwenda Kuswali Taraawiyh Kwa Kuvunja Amri Ya Mumewe
Mwanamke Kwenda Kuswali Tarawiyh Kwa Kuvunja Amri Ya Mumewe
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
SWALI:
Mwanamke akitoka kwenda kuswali Taraawiyh msikitini na mumewe hayuko radhi naye, kwani alimwambia aswali nyumbani atapata thawabu; je, Swalaah yake imesihi?
JIBU:
Tunamuambia mume usimzuie mkewe kwenda kuswali msikitini kwani Nabiy amekataza hivyo. Amesema: ((Msiwakataze wanawake kwenda katika nyumba za Allaah)) [Muslim]
Na tunamwambia mke: “Mtii mume wako maana bila shaka amekukataza kwa maslaha au khofu ya fitnah kama alivyosema kuwa Swalaah yako nyumbani ni bora kuliko msikitini kutokana na kauli ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ((Na nyumba zao ni bora kwao))”
[Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)]