07-Imaam Ibn ‘Uthaymiyn: Kuswali Taraawiyh Ramadhwaan Ni Lazima Aswali Mwezi Mzima?
Kuswali Taraawiyh Ramadhwaan Ni Lazima Aswali Mwezi Mzima?
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
SWALI:
Anayeanza kuswali Taraawiyh inampasa aendelee nayo Ramadhwaan nzima? (Au anaweza kuswali na kuacha?)
JIBU:
La! Si lazima aendelee nayo mwezi mzima kwa sababu ni Sunnah iliyosisitizwa ambayo akiswali atapata thawabu na akiacha hatokuwa na dhambi. Lakini kwa kuacha kuswali atakosa thawabu nyingi kama tulivyobainisha kabla.
[Imaam Ibn ‘Uthaymiyn - Fataawaa Ramadhwaan Mjalada 2, Uk 837 Fataawaa 831, Fiqh Al-'Ibadaat libni 'Uthaymiyn Uk. 205-206]