01-Imaam Ibn Baaz: Dawa Ya Mswaki Inabatilisha Swawm?
Dawa Ya Mswaki Inabatilisha Swawm?
Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah)
SWALI:
Je, dawa ya mswaki inabatilisha Swawm?
JIBU:
Dawa ya mswaki haibatilishi Swawm ikiwa atasafisha meno yake kisha ateme bila ya kuimeza. Ikiwa atameza kwa kukusudia, Swawm yake imebatilika.
[Mawqi’ Ar-Rasmiy – Imaam Ibn Baaz]
