03-Al-Lajnah Ad-Daaimah: Alisukutua Maji Baridi Akiwa Katika Swawm Kutokana Na Mdomo Kuwa Mkavu Mno

Alisukutua Maji Baridi Akiwa Katika Swawm Kutokana Na Mdomo Kuwa Mkavu Mno

 

 Al-Lajnah Ad-Daaimah

 

www.alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Nilikuwa mja mzito na hali ya hewa ilikuwa ni joto mno mdomo wangu ukawa umekauka, basi nikafanya madhwmadhwah (kusukutua) kwa maji ya baridi ili kuurutubisha mdomo wangu, lakini nilijitahadharisha kutokumeza maji. Je, nimefanya dhambi na je, nilipe kafara kwa hilo?

 

 

JIBU:

 

Kutokana na ulivyosema, hakuna dhambi juu yako na huwajibiki kulipa siku hiyo uliyofanya madhwmadhwah kwa maji kwa sababu haibatilishi swawm ya mtu.

 

 

Wa biLLaahi At-Tawfiyq wa Swalla Allaahu ‘alaa Nabiyyina Muhammad wa aalihi wa Swahbihi wa sallam.

 

 

[Fataawa Al-Lajnah Ad-Daaimah Lil Buhuwth Al-‘Ilmiyyah Wal Iftaa (20344)]

 

 

Share