04-Imaam Ibn ‘Uthaymiyn: Kujipaka Au Kunusa Mafuta Mazuri Akiwa Katika Swawm
Kujipaka Au Kunusa Mafuta Mazuri Akiwa Katika Swawm
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
SWALI:
Nini hukumu ya mtu aliyefunga na kutumia mafuta mazuri siku za Ramadhaan?
JIBU:
Hakuna ubaya kutumia na kunusa mafuta mazuri siku za Ramadhwaan isipokuwa kufukiza bukhuwr (udi) usikaribie hadi ukavuta pumzi za moshi na ukaingia tumboni.
[Imaam Muhammad bin Swaalih Ibn ‘Uthyamiyn - Fiqhul ‘Ibaadaat Uk. No. 217 Maktabatul-Iymaan]
