05-Imaam Ibn Qudaamah Al-Maddisiyy: Aliyesilimu Katika Ramadhwaan Anawajibika Swiyaam?
Aliyesilimu Katika Ramadhwaan Anawajibika Swiyaam?
Imaam Ibn Qudaamah Al-Maddisiyy
Al-Khiraqiy kasema:
"Ikiwa Kafiri atasilimu wakati wa Ramadhwaan, anatakiwa kufunga mwezi (masiku) yaliyobakia.
Ama kuhusu siku za mwezi huo zilizompita kabla hajakuwa Muislamu, sio waajib kwake kulipa siku hizo. Kauli hii ni ya Ash-Sha'biy, Qataadah, Maalik, Al-Awza'iy, Ash-Shaafi'iy, Abu Thawr na Hanafiyyah.
'Atwaa kasema analazimika kulipa siku hizo.
Kutoka kwa al-Hassan [Al-Baswriy] kumepokelewa kauli zote mbili.
Ama kuhusu sisi – Hanaabilah – hatuoni kama ni waajib kwake kulipa siku hizo ambazo zilipita hali ya kuwa alikuwa kafiri. Hali kadhalika si waajib kwake kulipa Ramadhwaan iliyopita.
[Al-Mughniy (4/414-415)]