15-Imaam Ibn ‘Uthaymiyn: Aliyefariki Katika Ramadhwaan Amaliziwe Swiyaam Siku Zilobakia
Aliyefariki Katika Ramadhwaan Amaliziwe Swiyaam Siku Zilobakia?
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
SWALI:
Ikiwa Muislamu alifunga baadhi ya siku katika Ramadhwaan kisha akafariki, je inampasa mtu mwenye jukumu la mambo yake (baada ya kufa kwake) ammalizie Swawm (ya siku zilizobakia za Ramadhwaan) kwa ajili yake?
JIBU:
Hapana! Haimpasi mwenye jukumu la mambo yake kummalizia Swawm (za siku zilizobakia za Ramadhwaan) kwa ajili yake wala kulisha masikini kwa ajili yake. Hii ni kwa sababu mtu anapofariki vitendo vyake vyote vinakatika kama alivyosema Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ((Mwana Aadam anapofariki ‘amali zake zote hukatika isipokuwa matatu: Swadaqah inayoendelea, elimu inayoendelea kunufaisha na mtoto mwema anayemuombea)).
Kwa kutokana na Hadiyth hii, mtu akifariki katika hali iliyotajwa katika Swali, haina haja amaliziwe siku zilizobakia za Ramadhwaan au kulisha masikini na wanaohitaji kwa ajili yake. Na hata kama alifariki katikati ya siku na alikuwa amefunga basi haina haja kumlipia siku ile wala kulisha masikini au watu wanaohitaji kwa siku ile kwa ajili yake.
[Imaam Ibn ‘Uthaymiyn - Fataawa Ramadhwaan – Mjalada 2, Ukurasa 645, Fatwa Namba 649; Fiqh al-Ibaadaat libni 'Uthaymiyn - Ukurasa 203]