Rolls Za Mdalasini Na Glaze Ya Icing Sugar
Rolls Za Mdalasini Na Glaze Ya Icing Sugar
Vipimo
Unga mweupe vikombe 4
Siagi vijiko vya kulia 2 ½ weka nje ya friji iyayuke
Hamira vijiko 2 vya kulia
Sukari vijiko 3 vya kulia
Maziwa ½ kikombe
Mazi ya vuguvugu (warm) ½ kikombe
Yai 1
Sukari ¼ kikombe
Chumvi ¼ kijiko cha chai
Mjazo Wa Rolls
Sukari ½ kikombe
Siagi (butter) vijiko 3 vya kulia weka nje ya friji iyayuke
Mdalasini wa unga kijiko 1 cha kulia
- Changanya sukari na mdalasini pamoja.
- Siagi tumilia kupaza katika donge baada ya kusukuma
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Rolls
- Washa oven lishike moto mdogo wa kiasi.
- Katika bakuli weka unga, sukari na hamira changanya vizuri.
- Changanya pamoja maziwa, siagi, yai, maji umimine katika bakuli.
- Changanya vizuri na unga na ukande vizuri unga uwe donge.
- Pakaza siagi katika bakuli jengine, uweke unga na ufunike wacha donge litulie na liumuke kiasi nusu saa takriban.
- Lisukumu donge liwe kubwa kisha pakaza siagi na nyunyizi mdalasini na sukari uliyochanganya.
- Zungusha donge kisha kata rolls kiasi zitokee 15
- Pakaza siagi katika treya na nyunyizia sukari.
- Panga rolls zikaribiane kushikana kisha acha ziumuke kiasi.
- Tia katika oven uchome (bake) kiasi dakika 30 takriban mpaka zigeuke rangi ya hudhurungi (golden brown)
Glaze Ya Icing Sugari Juu Ya Rolls
Sukari ya icing sugar vikombe 2 ½
Vanilla 1 kijiko cha chai
Maziwa mazito vijiko 4 vya kulia
Maziwa mazito vijiko 2 vya kulia
Siagi vijiko 4 vya kulia
- Changanya katika kibakuli siagi maziwa, icing sugar na vanilla ukoroge vizuri. Ikiwa nyepesi ongezea sukari ya icing tena.
- Nyunyizia juu ya rolls zikiwa tayari.
Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)