Keki Ya Nazi Na Semolina Kwa Shira Ya Mdalasini
Keki Ya Nazi Na Semolina Kwa Shira Ya Mdalasini
Vipimo
Nazi ya chenga kikombe 1
Unga wa sembe wa chenga (Semolina) 1
Vijiko 10 vya kulia
Sukari kikombe 1
Baking powder kijiko cha chai
Mtindi 1 kikombe
Maziwa mazito ¼ kikombe
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Andaa shira yake kwanza:
- Washa oven moto wa kiasi baina ya 300 – 350 Deg F
- Katika bakuli changanya sukari na mtindi mpaka ilainike.
- Tia unga wa sembe wa chenga (semolina), maziwa na baking powder.
- Pole pole tia siagi uliyoyayuka changanya vizuri.
- Funika uache mchanganyiko kidogo utulie.
- Mimina kwenye treya ya oven uliyopakaza siagi.
- Pika (bake) kiasi kwa muda dakika 40 takriban mpaka juu igeuke rangi ya hudhurungi na uhakikishe imewiva.
- Epua umwagie shira yake>
Shira
Sukari kikombe 1 ½
Maji kikombe 1 ¾
Mdalasini ½ kijiko cha chai
Ndimuu ½ kijiko cha chai
Changanya vizuri uchemshe hadi iwe nzito kisha acha ipoe ndio umwagi juu ya keki iyayuke ndani yake
Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)