11-Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Tofauti Ya Swalaah Ya Taraawiyh Na Swalaah Ya Qiyaam
Tofauti Baina Ya Swalaah Ya Taraawiyh Na Swalaah Ya Qiyaam
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
SWALI:
Nini Tofauti Ya Swalaah Ya Taraawiyh Ambayo ni baada ya Swalaah ya ‘Ishaa na Swalaah Ya Qiyaam Ambayo ni mwisho wa Usiku katika Ramadhwaan
JIBU:
Hakuna tofauti baina ya hizo mbili.
Swalaah ya Taraawiyh ima ni mwanzo wa usiku au mwisho wa usiku.
Lakini katika masiku ya mwisho ya Ramadhwaan, watu wanapenda kukesha usiku kufuata mwendo wa Rasuli (‘Alayhis-Swalaatu was-Salaam) kwa sababu alikuwa akiuhuisha usiku mzima katika masiku kumi ya mwisho.
Na kwa ajili hiyo, ndio (watu) wakakifanya Qiyaamu (kisimamo cha usiku) kuwa ni mwisho wa usiku.
Na Swalaah khafifu ambayo inaitwa Taraawiyh (huwa wanaiswali) mwanzo wa usiku. Na wala hakuna ubaya (kufanya) hivyo (kuswali mara mbili usiku kwa kuiswali moja mapema baada ya ‘Ishaa, na nyingine mwisho wa usiku).
[Silsilat Liqaat Al-Baab Al-Maftuwh, 107]