12-Al-Lajnah Ad-Daaimah: Bid’ah Za Ramadhwaan: Kumdhukuru Allaah Kila Baada Ya Rakaa Za Tarawiyh

Bid’ah Za Ramadhwaan: Kumdhukuru Allaah Kila Baada Ya Rakaa Za Taraawiyh

 

Al-Lajnah Ad-Daaimah

 

www.alhidaaya.com

 

 

Adkhaar au kumswalia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa pamoja baada ya kila Swalaah ya fardhi au Naafilah (Sunnah ya ziada) au baina ya Rakaa za Taraawiyh ni bid’ah ya kuzushwa na imethibiti kutoka kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwamba amesema:

 

((Atakayezusha katika jambo letu hili (Dini yetu) ambalo halimo basi litarudishwa))

 

 

[Fataawaa Al-Lajnah Ad-Daaimah (2529)]

 

 

Share