14-Imaam Ibn ‘Uthaymiyn : Zipi Nguzo Za I’tikaaf Na Sharti Zake? Na Je, Inasihi Bila Ya Swawm?

Zipi Nguzo Za I’tikaaf Na Sharti Zake? Na Je, Inasihi Bila Ya Swawm?

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

14-Zipi Nguzo Za I’tikaaf Na Sharti Zake? Na Je, Inasihi Bila Ya Swawm?

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:

 

a. Nguzo ya I’tikaaf ni kulazimika (kufanyika I’tikaaf) katika Msikiti kwa ajili ya utiifu kwa Allaah (‘Azza wa Jalla) katika kumwabudu Yeye, na kujikurubisha Kwake na kujipwekesha katika kumwabudu.

 

b. Ama sharti zake, basi ni kama zilivyo sharti za ‘ibaadah zote miongoni mwazo ni: Uislamu, akili, na inasihi kwa asiyebaleghe, na inasihi kwa mwanaume na mwanamke.

 

c. Na inasihi bila ya Swawm, na inasihi katika Misikiti yote.

 

[Majmuw’ Al-Fataawaa (20/162)]

 

 

 

Share